Sura ya 97 ya Qur'ani

Sura Al-Qadr

Makkiyya Aya 5 Juzuu 30
Al-Qadr

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

بِّسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ إِنَّآ أَنزَلْنَٰهُ فِى لَيْلَةِ ٱلْقَدْرِ ﴿١﴾

Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.

Tafsir al-Muyassar (Kiarabu)

وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا لَيْلَةُ ٱلْقَدْرِ ﴿٢﴾

Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?

Tafsir al-Muyassar (Kiarabu)

لَيْلَةُ ٱلْقَدْرِ خَيْرٌۭ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍۢ ﴿٣﴾

Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.

Tafsir al-Muyassar (Kiarabu)

تَنَزَّلُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍۢ ﴿٤﴾

Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.

Tafsir al-Muyassar (Kiarabu)

سَلَٰمٌ هِىَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ ٱلْفَجْرِ ﴿٥﴾

Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.

Tafsir al-Muyassar (Kiarabu)

Al-Qadr Aya 1 kati ya 5

Maandishi ya Kiarabu: hati ya Kiothmani. Tafsiri: Ali Muhsin Al-Barwani. Sauti: everyayah.com.

Kuhusu Sura Al-Qadr

Sura Al-Qadr (القدر) ni sura ya 97 ya Qur'ani. Ina aya 5 na iko katika Juzuu 30. Imeainishwa kama sura ya Makkiyya, yaani iliteremshwa zaidi kabla ya Mtume kuhama (Hijra) kwenda Madina.

Jina lake, القدر, ndivyo sura hii inavyojulikana kwa Kiarabu.

Maswali kuhusu Sura Al-Qadr

Sura Al-Qadr ina aya ngapi?

Sura Al-Qadr ina aya 5.

Je, Sura Al-Qadr ni ya Makkiyya au Madaniyya?

Uainishaji: Makkiyya.

Sura Al-Qadr iko katika Juzuu ipi?

Sura Al-Qadr iko katika Juzuu 30.

Naweza kusikiliza Sura Al-Qadr wapi?

Bonyeza Cheza kwenye ukurasa huu kuisikia aya kwa aya, ikisomwa na Abdur-Rahman As-Sudais, Mishary Alafasy, Mahmoud Khalil Al-Husary, Abdul Basit Abdus-Samad, Maher Al-Muaiqly, Saad Al-Ghamdi, Ahmad Al-Ajmi, Abu Bakr Ash-Shatri, Hani Ar-Rifai, Mohamed Siddiq Al-Minshawi, Ali Al-Hudhaify, Muhammad Ayyub, Abdullah Basfar, Yasser Ad-Dosari, Nasser Al-Qatami, Salah Al-Budair, Saud Ash-Shuraim, Abdullah Awad Al-Juhany, Muhammad Jibreel.

This page is translated with machine assistance and may contain mistakes. The English and Arabic versions are our reference. About our sources