Mtu wa ukweli
Allah anamwita Idris mtu wa ukweli na mtume, anasema alimpandisha hadi daraja ya juu, na anamhesabu miongoni mwa wasubirifu na wema.
Onyesha aya (4)
وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَٰبِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ صِدِّيقًۭا نَّبِيًّۭا ﴿٥٦﴾
Na mtaje katika Kitabu Idris. Hakika yeye alikuwa ni mkweli Nabii.
وَرَفَعْنَٰهُ مَكَانًا عَلِيًّا ﴿٥٧﴾
Na tulimuinua daraja ya juu.
وَإِسْمَٰعِيلَ وَإِدْرِيسَ وَذَا ٱلْكِفْلِ ۖ كُلٌّۭ مِّنَ ٱلصَّٰبِرِينَ ﴿٨٥﴾
Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli - wote walikuwa miongoni mwa wanao subiri.
وَأَدْخَلْنَٰهُمْ فِى رَحْمَتِنَآ ۖ إِنَّهُم مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ ﴿٨٦﴾
Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema.