Meli na samaki
Yunus anakimbilia meli iliyojaa. Wanapiga kura naye yumo miongoni mwa walioshindwa, na samaki anammeza akiwa mwenye kulaumiwa. Kama asingekuwa miongoni mwa wanaomtukuza Allah, angebaki tumboni mwake hadi Siku watakayofufuliwa. Anatupwa kwenye pwani tupu, akiwa mgonjwa, na mmea wa mung'unye unamea juu yake.
Onyesha aya (10)
وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ ﴿١٣٩﴾
Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.
إِذْ أَبَقَ إِلَى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ ﴿١٤٠﴾
Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.
فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُدْحَضِينَ ﴿١٤١﴾
Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa.
فَٱلْتَقَمَهُ ٱلْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌۭ ﴿١٤٢﴾
Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.
فَلَوْلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُسَبِّحِينَ ﴿١٤٣﴾
Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,
لَلَبِثَ فِى بَطْنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٤٤﴾
Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.
۞ فَنَبَذْنَٰهُ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٌۭ ﴿١٤٥﴾
Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.
وَأَنۢبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةًۭ مِّن يَقْطِينٍۢ ﴿١٤٦﴾
Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye.
وَأَرْسَلْنَٰهُ إِلَىٰ مِا۟ئَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ ﴿١٤٧﴾
Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.
فَـَٔامَنُوا۟ فَمَتَّعْنَٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍۢ ﴿١٤٨﴾
Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.