Fadhila za kumkumbuka Allah
قَالَ صلى الله عليه وسلم مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ فِي يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ حُطَّتْ خَطَايَاهُ وَلَوْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْر)).
(Atakayesema:(Ametakasika Allah na namsifu.) mara mia moja kwa siku, madhambi yake hufutwa, hata kama yanafanana na povu la bahari.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ عَشْرَ مِرَارٍ، كَانَ كَمَنْ أَعْتَقَ أَرْبَعَةَ أَنْفُسٍ مِنْ وَلَدِ إِسْمَاعِيلَ)).
(Abu Hurayrah alisimulia kwamba Mtume wa Allah alisema: ‘Atakayesema: (Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah peke yake, hana mshirika. Ni Wake ufalme wote na sifa zote na Yeye ni Muweza wa kila kitu.) mara mia moja kwa siku, atapata malipo ya kuwaachia huru watumwa kumi, anaandikiwa mema mia moja na kufutiwa maovu mia moja na atapata kinga dhidi ya shetani siku hiyo hadi jioni, na hakuna atakayekuja na lililo bora kuliko hilo isipokuwa mtu aliyefanya zaidi.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلَى اللِّسَانِ، ثَقِيلَتَانِ فِي الْمِيزَانِ، حَبِيبَتَانِ إِلَى الرَّحْمَنِ: سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ، سُبْحانَ اللَّهِ الْعَظِيمِ)).
(Abu Hurayrah alisimulia kwamba Mtume wa Allah alisema:’(Kuna) Maneno mawili, (ambayo ni) mepesi ulimini, mazito katika Mizani na yanayopendwa na Mwingi wa rehema: (Ametakasika Allah na namsifu. Ametakasika Allah, Mkuu kabisa.))
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((لَأَنْ أَقُولَ سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمسُ)).
(Abu Hurayrah alisimulia kwamba Mtume wa Allah alisema: ‘Kusema: (Ametakasika Allah, na sifa zote njema ni za Allah. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah, na Allah ni Mkubwa kuliko vyote.) kunapendeza zaidi kwangu kuliko kila kitu ambacho jua limechomoza juu yake.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((أَيَعْجِزُ أَحَدُكُم أَنْ يَكْسِبَ كُلَّ يَوْمٍ أَلْفَ حَسَنَةٍ)) فَسَأَلَهُ سَائِلٌ مِنْ جُلَسَائِهِ كَيْفَ يَكْسِبُ أَحَدُنَا أَلْفَ حَسَنَةٍ؟ قَالَ: ((يُسَبِّحُ مِائَةَ تَسْبِيحَةٍ، فَيُكتَبُ لَهُ أَلْفُ حَسَنَةٍ أَوْ يُحَطُّ عَنْهُ أَلْفُ خَطِيئَةٍ)).
(Sa’d alisema: ‘Tulikuwa tumekaa na Mtume wa Allah, naye akasema: ‘Je, yupo kati yenu asiyeweza kupata mema elfu moja kila siku?’ Mtu mmoja akamuuliza: Mtu anawezaje kupata mema elfu moja? Akajibu: ‘Aseme: (Ametakasika Allah.) mara mia moja, kwani ataandikiwa mema elfu moja au kufutiwa maovu elfu moja.)
((مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللَّهِ الْعَظِيمِ وَبِحَمْدِهِ غُرِسَتْ لَهُ نَخْلَةٌ فِي الْجَنَّةِ)).
(Jabir alisimulia kwamba Nabii alisema: ‘Atakayesema: (Ametakasika Allah, Mkuu kabisa, na namsifu.) atapandikiwa mtende Peponi.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((يَا عَبْدَ اللَّهِ بْنَ قَيْسٍ أَلاَ أَدُلُّكَ عَلَى كَنْزٍ مِنْ كُنُوزِ الْجَنَّةِ))؟ فَقُلْتُ: بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: ((قُلْ لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ)).
(‘Abdullah bin Qays alisimulia kwamba Nabii alimwambia: ‘Ewe ‘Abdullah bin Qays, je, nikujulishe hazina miongoni mwa hazina za Peponi?’ Kisha akasema: ‘Sema: (Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Allah.))
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((أَحَبُّ الْكَلاَمِ إِلَى اللَّهِ أَرْبَعٌ: سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، لاَ يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأتَ)).
(maneno yanayopendwa zaidi na Allah ni manne: (Ametakasika Allah, sifa zote njema ni za Allah. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah na Allah ni Mkubwa kuliko vyote.))(haijalishi uanze na lipi kati yake.)
جَاءَ أَعْرَابِيٌّ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ: عَلِّمْنِي كَلاماً أَقُولُهُ: قَالَ: ((قُلْ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيراً، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثِيراً، سُبْحَانَ اللَّهِ رَبِّ العَالَمِينَ، لاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ)) قَالَ: فَهَؤُلاَءِ لِرَبِّي، فَمَا لِي؟ قَالَ: ((قُلْ: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي، وَارْحَمْنِي، وَاهْدِنِي، وَارْزُقْنِي)).
(Sa‘d bin Abi Waqqas alisimulia kwamba mtu mmoja alimjia Mtume wa Allah na kumwambia: ‘Nifundishe kitu cha kukisema?’ Akasema: ‘Sema: (Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah peke yake, hana mshirika. Allah ni Mkubwa kabisa na sifa nyingi ni za Allah. Ametakasika Allah, Mola wa walimwengu. Hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Allah, Mtukufu, Mwenye hekima.) kisha mtu huyo akasema: ‘Haya ni kwa ajili ya Mola wangu, na kwa ajili yangu ni nini?’ Akajibu: ‘Sema:(Ewe Allah, nisamehe, unirehemu, uniongoze na uniruzuku.))
كَانَ الرَّجُلُ إِذَا أَسْلَمَ عَلَّمَهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم الصَّلاَةَ ثُمَّ أَمَرَهُ أَنْ يَدْعُوَ بِهَؤُلاَءِ الْكَلِمَاتِ: ((اللَّهُمَّ اغْفِرِ لِي، وَارْحَمْنِي، وَاهْدِنِي، وَعَافِنِي وَارْزُقْنِي)).
(Tariq Al-Ashja‘i alisema: ‘Mtu alipokuwa akisilimu, Mtume alikuwa akimfundisha jinsi ya kuswali kisha akimwamuru aombe dua kwa maneno yafuatayo: (Ewe Allah, nisamehe, unirehemu, uniongoze, unipe afya na uniruzuku.))
((إِنَّ أَفْضَلَ الدُّعَاءِ الْحَمْدُ لِلَّهِ، وَأَفْضَلَ الذِّكْرِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ)).
(Jabir bin ‘Abdillah alisimulia kwamba Mtume wa Allah alisema: ‘Hakika, dua bora kabisa ni: (Sifa zote njema ni za Allah.) na hakika, dhikri bora kabisa ni: (Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah.))
الباقيات الصالحات : سبحان الله والحمد لله ، ولا إله إلا الله ،والله أكبر ،و لا حول ولا قوة إلا بالله
Mema yanayobaki ni ‘Ametukuka Allah’, na ‘Sifa njema ni za Allah’, na ‘Hakuna anayestahiki kuabudiwa ila Allah’, na ‘Allah ni Mkubwa kuliko vyote’, na ‘Hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa Allah’