Cha kusema kabla ya kulala
((يَجْمَعُ كَفَّيْهِ ثُمَّ يَنْفُثُ فِيهِمَا فَيَقْرَأُ فِيهِمَا:بسم الله الرحمن الرحيم ﴿قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ اللَّهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُواً أَحَدٌ﴾. بسم الله الرحمن الرحيم ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ مِن شَرِّ مَا خَلَقَ وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ﴾. بسم الله الرحمن الرحيم ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ مَلِكِ النَّاسِ إِلَهِ النَّاسِ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ مِنَ الْجِنَّةِ وَ النَّاسِ﴾ ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقبَلَ مِنْ جَسَدِهِ)) (يفعلُ ذلك ثلاثَ مرَّاتٍ).
(Kila usiku alipokwenda kitandani, Mtume alikuwa akiunganisha viganja vyake, akipuliza ndani yake (kupuliza kwa hewa zaidi na mate kidogo sana), kisha akisoma sura tatu za mwisho za Qur'an (Al-Ikhlas, Al-Falaq, An-Nas) kisha akijipangusa mwili wake wote kadiri awezavyo kwa mikono yake, akianzia kichwani na usoni kisha sehemu zote za mwili, na alikuwa akifanya hivyo mara tatu.)
﴿اللَّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْـــــــــــدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ﴾.
Allah - hakuna mungu isipokuwa Yeye, Aliye Hai, Msimamizi wa [kila] kilichopo. Hapatwi na usingizi mwepesi wala usingizi mzito. Ni Wake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Nani awezaye kuombea mbele Yake isipokuwa kwa idhini Yake? Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, nao hawakizunguki chochote katika ujuzi Wake isipokuwa kwa alichokitaka. Kursi Yake imeenea mbingu na ardhi, na kuvihifadhi hakumchoshi. Naye ndiye Aliye Juu, Mkuu kabisa.
﴿آمَنَ الرَّسُولُ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِ وَالْمُؤْمِنُونَ كُلٌّ آمَنَ بِاللَّهِ وَمَلآئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ لاَ نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِ وَقَالُواْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ لاَ يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْساً إِلاَّ وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبَتْ رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْراً كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَآ أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ﴾.
( 285 ) Mtume ameamini yale aliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wake, na waumini [pia]. Wote wameamini Allah na Malaika Wake na Vitabu Vyake na Mitume Wake, [wakisema], Hatubagui kati ya yeyote katika Mitume Wake. Na wakasema, Tumesikia na tumetii. [Tunaomba] msamaha Wako, Ewe Mola wetu, na marejeo ni Kwako. ( 286 ) Allah haitwiki nafsi yoyote isipokuwa [kwa] kile kilicho katika uwezo wake. Itapata [malipo ya] [mema] iliyoyachuma, na itabeba [adhabu ya] [maovu] iliyoyachuma. Ewe Mola wetu, usituhukumu kwa makosa tukisahau au tukikosea. Ewe Mola wetu, wala usitubebeshe mzigo mzito kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Ewe Mola wetu, wala usitutwike tusiloliweza. Na utusamehe; na utughufirie; na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu, basi tupe ushindi dhidi ya watu makafiri.
((بِاسْمِكَ رَبِّي وَضَعْتُ جَنْبِي، وَبِكَ أَرْفَعُهُ، فَإِن أَمْسَكْتَ نَفْسِي فارْحَمْهَا، وَإِنْ أَرْسَلْتَهَا فَاحْفَظْهَا، بِمَا تَحْفَظُ بِهِ عِبَادَكَ الصَّالِحِينَ)).
(Kwa jina Lako, Ewe Mola wangu, nalala na kwa jina Lako naamka, basi ukiichukua nafsi yangu iirehemu, na ukiirudisha ilinde kama unavyowalinda waja Wako wema.)
((اللَّهُمَّ إِنَّكَ خَلَقْتَ نَفْسِي وَأَنْتَ تَوَفَّاهَا، لَكَ مَمَاتُهَا وَمَحْياهَا، إِنْ أَحْيَيْتَهَا فَاحْفَظْهَا، وَإِنْ أَمَتَّهَا فَاغْفِرْ لَهَا. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ العَافِيَةَ)).
(Ewe Allah, hakika Wewe umeiumba nafsi yangu na Wewe utaichukua roho yake, ni Yako uhai wake na kifo chake. Ukiihuisha basi ilinde, na ukiichukua roho yake basi isamehe. Ewe Allah, nakuomba afya njema.)
((اللَّهُمَّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ عِبَادَكَ)).
(Ewe Allah, nilinde na adhabu Yako siku waja Wako watakapofufuliwa.)
((بِاسْمِكَ اللَّهُمَّ أَمُوتُ وَأَحْيَا)).
(Kwa jina Lako, Ewe Allah, naishi na nafariki.)
((سُبْحَانَ اللَّهِ (ثلاثاً وثلاثين) وَالْحَمْدُ لِلَّهِ (ثلاثاً وثلاثين) وَاللَّهُ أَكْبَرُ (أربعاً وثلاثينَ))).
(Ametakasika Allah. (mara thelathini na tatu) Sifa zote njema ni za Allah.(mara thelathini na tatu) Allah ni Mkubwa kuliko vyote.(mara thelathini na nne))
((اللَّهُمَّ رَبَّ السَّمَوَاتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الأَرْضِ، وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ، رَبَّنَا وَرَبَّ كُلِّ شَيْءٍ، فَالِقَ الْحَبِّ وَالنَّوَى، وَمُنْزِلَ التَّوْرَاةِ وَالْإِنْجِيلِ، وَالْفُرْقَانِ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ كُلِّ شَيْءٍ أَنْتَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهِ. اللَّهُمَّ أَنْتَ الأَوَّلُ فَلَيْسَ قَبْلَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الآخِرُ فَلَيسَ بَعْدَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الظَّاهِرُ فَلَيْسَ فَوْقَكَ شَيْءٌ، وَأَنْتَ الْبَاطِنُ فَلَيْسَ دُونَكَ شَيْءٌ، اقْضِ عَنَّا الدَّيْنَ وَأَغْنِنَا مِنَ الْفَقْرِ)).
(Ewe Allah, Mola wa mbingu saba na Arshi tukufu, Mola wetu na Mola wa kila kitu, Mpasuaji wa mbegu na kokwa ya tende, Mteremshaji wa Tawrati, Injili na Furqani, najikinga kwako kutokana na shari ya kila kitu ambacho Wewe unakishika kwa utosi wake (yaani una mamlaka kamili juu yake). Ewe Allah, Wewe ndiye wa Kwanza hivyo hakuna kitu kabla Yako, na Wewe ndiye wa Mwisho hivyo hakuna kitu baada Yako. Wewe ndiye Adh-Dhahir hivyo hakuna kitu juu Yako, na Wewe ndiye Al-Batin hivyo hakuna kitu kilicho karibu zaidi kuliko Wewe. Tulipie deni letu na utuepushe na ufakiri.)(Tawrati: Kitabu alichoteremshiwa Musa u.)(Injili: Kitabu alichoteremshiwa Isa u.)(Furqani: Moja ya majina mengi ya Qur'an, maana yake: Kipambanuzi kinachotofautisha haki na batili.)(Adh-Dhahir: Inaashiria ukuu wa sifa Zake na udogo wa kila kiumbe mbele ya ukuu Wake na Utukufu Wake, kwani Yeye yuko juu ya viumbe Vyake vyote kwa dhati na sifa Zake.)(Al-Batin: Inaashiria ujuzi na ufahamu Wake wa siri zote, ya yaliyomo mioyoni na mambo ya ndani kabisa, kama inavyoashiria ukaribu Wake na kila kitu kwa namna inayoliwiana na utukufu Wake.)
((الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَطْعَمَنَا وَسَقَانَا، وَكَفَانَا، وَآوَانَا، فَكَمْ مِمَّنْ لاَ كَافِيَ لَهُ وَلاَ مُؤْوِيَ)).
(Sifa zote njema ni za Allah, Aliyetulisha na kutunywesha, na Aliyetutosheleza na kutupa makazi, kwani ni wengi wasio na wa kuwatosheleza wala wa kuwapa makazi.)
((اللَّهُمَّ عَالِمَ الغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَاطِرَ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ، رَبَّ كُلِّ شَيْءٍ وَمَلِيكَهُ، أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ نَفْسِي، وَمِنْ شَرِّ الشَّيْطانِ وَشِرْكِهِ، وَأَنْ أَقْتَرِفَ عَلَى نَفْسِي سُوءاً، أَوْ أَجُرَّهُ إِلَى مُسْلِمٍ)).
(Ewe Allah, Mjuzi wa yaliyofichika na yanayoonekana, Muumbaji wa mbingu na ardhi, Mola na Mfalme wa kila kitu, nashuhudia kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe. Najikinga kwako kutokana na shari ya nafsi yangu na kutokana na shari ya shetani na ushirikina wake, na kutokana na kuidhulumu nafsi yangu au kumsababishia Muislamu mwingine dhuluma hiyo.)(shirk (ushirikina): kumshirikisha mwingine na Allah katika yale yaliyo mahsusi kwake. Hili laweza kutokea katika (1) imani, mf. kuamini kuwa asiyekuwa Allah ana uwezo wa kunufaisha au kudhuru, (2) maneno, mf. kuapa kwa asiyekuwa Allah na (3) vitendo, mf. kurukuu au kusujudu kwa asiyekuwa Allah.)
((يَقْرَأُ ﴿الم﴾ تَنْزِيلَ السَّجْدَة ِ، وَتَبَارَكَ الَّذي بِيَدِهِ الْمُلْكُ)).
(Mtume hakuwa akilala mpaka asome Surat As-Sajdah (sura ya 32) na Surat Al-Mulk (sura ya 67).)
((اللَّهُمَّ أَسْلَمْتُ نَفْسِي إِلَيْكَ، وَفَوَّضْتُ أَمْرِي إِلَيْكَ، وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ، وَأَلْجَأْتُ ظَهْرِي إِلَيْكَ، رَغْبَةً وَرَهْبَةً إِلَيْكَ، لاَ مَلْجَأَ وَلاَ مَنْجَا مِنْكَ إِلاَّ إِلَيْكَ، آمَنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَ، وَبِنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ)).
(Ewe Allah, nakusalimisha nafsi yangu, na nakukabidhi jambo langu, na nakuelekezea uso wangu, na nakutegemea kikamilifu, kwa matumaini na kwa hofu juu Yako. Hakika hakuna kimbilio wala pa kuokoka kutoka Kwako isipokuwa kwako. Naamini Kitabu Chako ulichokiteremsha na Mtume Wako uliyemtuma.)(Ukifa basi utakufa juu ya fitra.)(fitra: dini ya Uislamu, njia ya Ibrahimu u.)
Dua unapoamka
(.الْحَمْدُ للَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا، وَإِلَيْهِ النُّشُورُ )
(Sifa zote njema ni za Allah ambaye ametuhuisha baada ya kutuchukulia uhai wetu, na kwake ndiko kufufuliwa.)
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَريكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ للَّهِ، وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكبَرُ، وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ الْعَلِيِّ الْعَظِيمِ، رَبِّ اغْفرْ لِي
(Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah peke yake, hana mshirika, ni Wake ufalme na sifa zote na Yeye ni Muweza wa kila kitu. Ametakasika Allah, na sifa zote njema ni za Allah, na hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah, Allah ni Mkubwa kuliko vyote na hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa kwa Allah, Aliye Juu, Mkuu kabisa. Ewe Mola wangu nisamehe)
( الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي عَافَانِي فِي جَسَدِي، وَرَدَّ عَلَيَّ رُوحِي، وَأَذِنَ لي بِذِكْرِهِ )
(Sifa zote njema ni za Allah ambaye amenirudishia afya yangu na kunirudishia roho yangu na kuniruhusu nimkumbuke.)
﴿ إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَاخْتِلاَفِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لأُوْلِي الألْبَابِ الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّهَ قِيَاماً وَقُعُوداً وَعَلَىَ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَذا بَاطِلاً سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِياً يُنَادِي لِلإِيمَانِ أَنْ آمِنُواْ بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الأبْرَارِ رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَى رُسُلِكَ وَلاَ تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّكَ لاَ تُخْلِفُ الْمِيعَادَ فَاسْتَجَابَ لَهُمْ رَبُّهُمْ أَنِّي لاَ أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَى بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ فَالَّذِينَ هَاجَرُواْ وَأُخْرِجُواْ مِن دِيَارِهِمْ وَأُوذُواْ فِي سَبِيلِي وَقَاتَلُواْ وَقُتِلُواْ لأُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلأُدْخِلَنَّهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ ثَوَاباً مِّن عِندِ اللَّهِ وَاللَّهُ عِندَهُ حُسْنُ الثَّوَابِ لاَ يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ الَّذِينَ كَفَرُواْ فِي الْبِلاَدِ مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ الْمِهَادُ لَكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْاْ رَبَّهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا نُزُلاً مِّنْ عِندِ اللَّهِ وَمَا عِندَ اللَّهِ خَيْرٌ لِّلأَبْرَارِ وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّهِ لاَ يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ ثَمَناً قَلِيلاً أُوْلَئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ إِنَّ اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اصْبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَاتَّقُواْ اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴾
( 190 ) Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kupishana usiku na mchana ziko ishara kwa wenye akili.( 191 ) Ambao humkumbuka Allah wakisimama na wakikaa na [wakiwa wamelala] ubavuni mwao na hutafakari juu ya uumbaji wa mbingu na ardhi, [wakisema], Ewe Mola wetu, hukuviumba hivi bure; Umetukuka Wewe [kutokana na jambo hilo]; basi tulinde na adhabu ya Moto.( 192 ) Ewe Mola wetu, hakika yeyote Utakayemuingiza Motoni - umemfedhehesha, na waovu hawana wasaidizi.( 193 ) Ewe Mola wetu, hakika sisi tumesikia mwitaji anayeita kwenye imani, [akisema], ‘Mwamini Mola wenu,’ nasi tumeamini. Ewe Mola wetu, basi tusamehe madhambi yetu na utuondolee maovu yetu na utufishe pamoja na watu wema.( 194 ) Ewe Mola wetu, na utupe ulichotuahidi kupitia Mitume Wako na usitufedheheshe Siku ya Kiyama. Hakika Wewe huvunji [ahadi Yako].( 195 ) Na Mola wao akawajibu, Sitapoteza kamwe kitendo cha mtendaji [yeyote] miongoni mwenu, awe mwanamume au mwanamke; nyinyi ni wa wenzenu. Basi wale waliohama au waliotolewa katika nyumba zao au waliodhuriwa katika njia Yangu au walipigana au waliuawa - bila shaka nitawafutia maovu yao, na bila shaka nitawaingiza katika bustani zipitazo mito chini yake kuwa ni malipo kutoka kwa Allah, na Allah ana kwake malipo mazuri zaidi.( 196 ) Wasikudanganye [mwendo wa uhuru] wa makafiri katika nchi.( 197 ) [Ni] starehe ndogo tu; kisha makazi yao [ya mwisho] ni Jahannamu, na ni mahali pabaya pa kupumzikia.( 198 ) Lakini wale waliomcha Mola wao watapata bustani zipitazo mito chini yake, wakikaa humo milele, kuwa ni makaribisho kutoka kwa Allah. Na yaliyo kwa Allah ni bora kwa wema.( 199 ) Na hakika miongoni mwa Watu wa Kitabu wapo wanaomwamini Allah na yale yaliyoteremshwa kwenu na yaliyoteremshwa kwao, [wakiwa] wanyenyekevu kwa Allah. Hawauzi aya za Allah kwa thamani ndogo. Hao watapata malipo yao kwa Mola wao. Hakika Allah ni Mwepesi wa kuhesabu.( 200 ) Enyi mlioamini, subirini na vumilieni na simameni imara na mcheni Allah ili mpate kufanikiwa.