Maneno ya dhikr ya asubuhi na jioni
أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيطَانِ الرَّجِيمِ ﴿اللَّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ لاَ تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلاَ نَوْمٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِنْدَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلاَ يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلاَّ بِمَا شَاء وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضَ وَلاَ يَؤُودُهُ حِفْظُهُمَا وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ﴾.
Allah - hakuna mungu isipokuwa Yeye, Aliye Hai, Msimamizi wa [kila] kilichopo. Hapatwi na usingizi mwepesi wala usingizi mzito. Ni Wake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Nani awezaye kuombea mbele Yake isipokuwa kwa idhini Yake? Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, nao hawakizunguki chochote katika ujuzi Wake isipokuwa kwa alichokitaka. Kursi Yake imeenea mbingu na ardhi, na kuvihifadhi hakumchoshi. Naye ndiye Aliye Juu, Mkuu kabisa.
(بسم الله الرحمن الرحيم ﴿قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ اللَّهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُواً أَحَدٌ﴾.) (بسم الله الرحمن الرحيم ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ مِن شَرِّ مَا خَلَقَ وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ﴾.) (بسم الله الرحمن الرحيم ﴿قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ مَلِكِ النَّاسِ إِلَهِ النَّاسِ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ مِنَ الْجِنَّةِ وَ النَّاسِ﴾)
([Sura Al-Ikhlas (112)]( 1 ) Sema, Yeye ni Allah, [ambaye ni] Mmoja,( 2 ) Allah, Tegemewa wa milele.( 3 ) Hakuzaa wala hakuzaliwa,( 4 ) Wala hana yeyote anayelingana naye.)([Sura Al-Falaq (113)] ( 1 ) Sema, Najikinga kwa Mola wa mwangaza wa asubuhi( 2 ) Kutokana na shari ya alivyoviumba( 3 ) Na kutokana na shari ya giza linapoingia( 4 ) Na kutokana na shari ya wapulizao mafundoni( 5 ) Na kutokana na shari ya hasidi anapohusudu. )([Sura An-Nas (114)])( 1 ) Sema, Najikinga kwa Mola wa wanadamu,( 2 ) Mfalme wa wanadamu.( 3 ) Mungu wa wanadamu,( 4 ) Kutokana na shari ya mwenye kutia wasiwasi anayejificha -( 5 ) Anayetia wasiwasi [maovu] vifuani mwa wanadamu -( 6 ) Miongoni mwa majini na wanadamu.
((أَصْبَحْنَا وَأَصْبَحَ الْمُلْكُ لِلَّهِ ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، لاَ إِلَهَ إلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، رَبِّ أَسْأَلُكَ خَيْرَ مَا فِي هَذَا الْيَوْمِ وَخَيرَ مَا بَعْدَهُ ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا فِي هَذَا الْيَوْمِ وَشَرِّ مَا بَعْدَهُ، رَبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْكَسَلِ وَسُوءِ الْكِبَرِ، رَبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابٍ فِي النَّارِ وَعَذَابٍ فِي الْقَبْرِ)). [ وإذا أمسى قال: أمسينا وأمسى الملك للَّه] [وإذا أمسى قال: رب أسألك خير ما في هذه الليلة، وخير ما بعدها، وأعوذ بك من شر ما في هذه الليلة، وشر ما بعدها.]
‘Tumefika asubuhi na wakati huu huu ufalme wote ni wa Allah, na sifa zote njema ni za Allah. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah peke yake, hana mshirika, ni Wake ufalme wote na sifa zote na Yeye ni Muweza wa kila kitu. Mola wangu, nakuomba kheri ya siku hii na kheri ya inayofuata, na najikinga kwako kutokana na shari ya siku hii na shari ya inayofuata. Mola wangu, najikinga kwako kutokana na uvivu na uzee wa kupindukia. Mola wangu, najikinga kwako kutokana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi.’
((اللَّهُمَّ بِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ أَمْسَيْنَا ، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوتُ وَإِلَيْكَ النُّشُورُ)). [وإذا أمسى قال: اللَّهم بك أمسينا، وبك أصبحنا، وبك نحيا، وبك نموت، وإليك المصير.]
(Ewe Allah, kwa idhini Yako tumefika asubuhi na kwa idhini Yako tumefika jioni, kwa idhini Yako tunaishi na tunakufa na kwako ndiko kufufuliwa kwetu.)[Jioni:](Ewe Allah, kwa idhini Yako tumefika jioni na kwa idhini Yako tumefika asubuhi, kwa idhini Yako tunaishi na tunakufa na kwako ndiko marejeo yetu.)
((اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لَا إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي فَإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنوبَ إِلاَّ أَنْتَ)).
(Ewe Allah, Wewe ndiye Mola wangu, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe, Umeniumba na mimi ni mja Wako na ninashikilia agano Lako na ahadi Yako kadiri ya uwezo wangu, najikinga kwako kutokana na shari ya niliyoyatenda. Nakiri neema Yako juu yangu na nakiri dhambi yangu, basi nisamehe, kwani hakika hakuna anayesamehe dhambi isipokuwa Wewe.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَصْبَحْتُ أُشْهِدُكَ، وَأُشْهِدُ حَمَلَةَ عَرْشِكَ، وَمَلاَئِكَتِكَ، وَجَمِيعَ خَلْقِكَ، أَنَّكَ أَنْتَ اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ وَحْدَكَ لاَ شَرِيكَ لَكَ، وَأَنَّ مُحَمَّداً عَبْدُكَ وَرَسُولُكَ)) (أربعَ مَرَّاتٍ).[ وإذا أمسى قال: اللَّهم إني أمسيت...]
(Ewe Allah, hakika nimefika asubuhi na nakuita Wewe, wabeba Arshi Yako, Malaika Wako, na viumbe Vyako vyote kuwa mashahidi kwamba Wewe ni Allah, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe, peke yako, huna mshirika na kwamba Muhammad ni Mja Wako na Mtume Wako.) (mara nne asubuhi na jioni)(Kumbuka: jioni, mtu husoma (amsaytu) badala ya (asbahtu).)
((اللَّهُمَّ مَا أَصْبَحَ بِي مِنْ نِعْمَةٍ أَوْ بِأَحَدٍ مِنْ خَلْقِكَ فَمِنْكَ وَحْدَكَ لاَ شَرِيكَ لَكَ، فَلَكَ الْحَمْدُ وَلَكَ الشُّكْرُ)). [وإذا أمسى قال: اللَّهم ما أمسى بي...]
(Ewe Allah, neema yoyote niliyoamkia mimi au kiumbe chochote Chako, ni kutoka Kwako peke yako, huna mshirika, basi ni Zako sifa zote na ni Kwako shukrani zote.)(…atakayesema haya asubuhi basi amekwisha kutoa shukrani za siku yake, na atakayesema haya jioni basi amekwisha kutoa shukrani za usiku wake.)(Kumbuka: jioni, mtu husoma (amsa) badala ya (asbaha).)
((اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَدَنِي، اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي سَمْعِي، اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَصَرِي، لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْكُفْرِ، وَالفَقْرِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ القَبْرِ، لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ)) (ثلاثَ مرَّاتٍ).
(Ewe Allah, nipe afya mwilini mwangu, Ewe Allah, nipe afya masikioni mwangu, Ewe Allah, nipe afya machoni mwangu. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe.)(mara tatu) (Ewe Allah, najikinga kwako kutokana na ukafiri na ufakiri, na najikinga kwako kutokana na adhabu ya kaburi. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe. (mara tatu))
((حَسْبِيَ اللَّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ عَلَيهِ تَوَكَّلتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ)) (سَبْعَ مَرّاتٍ).
Allah ananitosha, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, juu Yake nimetegemea na Yeye ni Mola wa Arshi tukufu.’ (Isome mara saba kwa Kiarabu.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ وَالْعَافِيَةَ: فِي دِينِي وَدُنْيَايَ وَأَهْلِي، وَمَالِي، اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي، وَآمِنْ رَوْعَاتِي، اللَّهُمَّ احْفَظْنِي مِنْ بَينِ يَدَيَّ، وَمِنْ خَلْفِي، وَعَنْ يَمِينِي، وَعَنْ شِمَالِي، وَمِنْ فَوْقِي، وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِي)).
Ewe Allah, nakuomba msamaha na afya njema katika dunia hii na Akhera. Ewe Allah, nakuomba msamaha na afya njema katika mambo yangu ya dini na ya dunia, na katika familia yangu na mali yangu. Ewe Allah, nistiri aibu zangu na tuliza khofu yangu. Ewe Allah, nilinde kutoka mbele na nyuma, kulia na kushoto, na kutoka juu, na najikinga kwako nisije kumezwa na ardhi.
((اللَّهُمَّ عَالِمَ الغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَاطِرَ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ، رَبَّ كُلِّ شَيْءٍ وَمَلِيكَهُ، أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ نَفْسِي، وَمِنْ شَرِّ الشَّيْطانِ وَشَرَكِهِ، وَأَنْ أَقْتَرِفَ عَلَى نَفْسِي سُوءاً، أَوْ أَجُرَّهُ إِلَى مُسْلِمٍ)).
(Ewe Allah, Mjuzi wa yasiyoonekana na yanayoonekana, Muumbaji wa mbingu na ardhi, Mola na Mfalme wa kila kitu, nashuhudia kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe. Najikinga kwako kutokana na shari ya nafsi yangu na kutokana na shari ya shetani na ushirikina wake, na kutokana na kuidhulumu nafsi yangu au kumsababishia Muislamu mwingine dhuluma hiyo.)(shirk (ushirikina): kumshirikisha mwingine na Allah katika yale yaliyo mahsusi kwake. Hili laweza kutokea katika (1) imani, mf. kuamini kuwa asiyekuwa Allah ana uwezo wa kunufaisha au kudhuru, (2) maneno, mf. kuapa kwa asiyekuwa Allah na (3) vitendo, mf. kurukuu au kusujudu kwa asiyekuwa Allah.)
((بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لاَ يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلاَ فِي السّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ)) (ثلاثَ مرَّاتٍ).
(Kwa jina la Allah ambaye kwa jina Lake hakuna kinachodhuru ardhini wala mbinguni na Yeye ndiye Msikivu, Mjuzi.’(mara tatu))
((رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبَّاً، وَبِالْإِسْلاَمِ دِيناً، وَبِمُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم نَبِيّاً)) (ثلاثَ مرَّاتٍ).
(Nimeridhika na Allah kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini na Muhammad kuwa Mtume.’(mara tatu))
((يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ بِرَحْمَتِكَ أَسْتَغيثُ أَصْلِحْ لِي شَأْنِيَ كُلَّهُ وَلاَ تَكِلْنِي إِلَى نَفْسِي طَرْفَةَ عَيْنٍ)).
(Ewe Uliye Hai milele, Ewe Msimamizi wa vyote, kwa rehema Yako naomba msaada, nirekebishie mambo yangu yote na usiniache nijisimamie mwenyewe, hata kwa kupepesa kwa jicho.)
((أَصْبَحْنَا وَأَصْبَحَ الْمُلْكُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، اللَّهُـمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَ هَذَا الْيَوْمِ:فَتْحَهُ، وَنَصْرَهُ، وَنورَهُ، وَبَرَكَتَهُ، وَهُدَاهُ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا فِيهِ وَشَرِّ مَا بَعْدَهُ)). [وإذا أمسى قال: أمسينا وأمسى الملك للَّه ربّ العالمين اللَّهم إني أسألك خير هذه الليلة: فتحها، ونصرها، ونورها، وبركتها، وهداها، وأعوذ بك من شر ما فيها، وشر ما بعدها.]
(Tumefika asubuhi na wakati huu huu ufalme wote ni wa Allah, Mola wa walimwengu. Ewe Allah, nakuomba kheri ya siku hii, ushindi wake na fursa zake, nuru yake na baraka zake na uongofu wake, na najikinga kwako kutokana na shari ya siku hii na shari inayofuata.)[Kwa jioni, dua inasomwa hivi:](Tumefika jioni na wakati huu huu ufalme wote ni wa Allah, Mola wa walimwengu. Ewe Allah, nakuomba kheri ya usiku huu, ushindi wake na fursa zake, nuru yake na baraka zake na uongofu wake, na najikinga kwako kutokana na shari ya usiku huu na shari inayofuata.)
((أَصْبَحْنا عَلَى فِطْرَةِ الْإِسْلاَمِ، وَعَلَى كَلِمَةِ الْإِخْلاَصِ، وَعَلَى دِينِ نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم، وَعَلَى مِلَّةِ أَبِينَا إِبْرَاهِيمَ، حَنِيفاً مُسْلِماً وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشرِكِينَ)). [وإذا أمسى قال: أمسينا على فطرة الإسلام...]
(Tumeamka juu ya fitra ya Uislamu, na neno la imani safi, na juu ya dini ya Nabii wetu Muhammad na dini ya baba yetu Ibrahimu, ambaye alikuwa Muislamu mwenye imani ya kweli na hakuwa miongoni mwa wanaomshirikisha Allah.)(fitra: dini ya Uislamu, njia ya Ibrahimu u.)(Kumbuka: jioni, mtu husoma amsayna badala ya asbahna.)
((سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ)) (مائة مرَّةٍ).
(Ametakasika Allah na namsifu.)(mara mia moja)
((لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)) (عشرَ مرَّات) ، أَوْ (مرَّةً واحدةً عندَ الكَسَلِ).
(Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah peke yake, hana mshirika, ni Wake ufalme wote na sifa zote, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.)( [mara kumi au mara moja ukiwa mvivu])
((لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ)) (مائةَ مرَّةٍ إذا أصبحَ).
(Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah peke yake, hana mshirika, ni Wake ufalme wote na sifa zote, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.)((mara mia moja kila siku))
((سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ: عَدَدَ خَلْقِهِ، وَرِضَا نَفْسِهِ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ، وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ)) (ثلاثَ مرَّاتٍ إذا أصبحَ).
(Ametakasika Allah na namsifu kwa idadi ya viumbe Vyake na radhi Yake, na kwa uzito wa Arshi Yake, na wino wa maneno Yake.)(mara tatu)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ عِلْماً نَافِعاً، وَرِزْقاً طَيِّباً، وَعَمَلاً مُتَقَبَّلاً)) (إذا أصبحَ).
(Ewe Allah, nakuomba elimu yenye manufaa, riziki njema, na vitendo vinavyokubaliwa.)
((أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ)) (مِائَةَ مَرَّةٍ فِي الْيَوْمِ).
‘Namwomba Allah msamaha na narejea kwake kwa toba.’ [mara mia moja kwa siku]
((أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ)) (ثلاثَ مرَّاتٍ إذا أمسى).
(Najikinga kwa maneno kamilifu ya Allah kutokana na shari ya alichokiumba.)(mara tatu jioni)
((اللَّهُمَّ صَلِّ وَسَلِّمْ عَلَى نَبَيِّنَا مُحَمَّدٍ)) (عشرَ مرَّاتٍ).
‘Ewe Allah, mswalie na umpe amani Nabii wetu Muhammad.’ [mara kumi]