((اللَّهُمَّ إِنِّي عَبْدُكَ، ابْنُ عَبْدِكَ، ابْنُ أَمَتِكَ، نَاصِيَتِي بِيَدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ، أَسْأَلُكَ بِكُــــلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ، سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَداً مِنْ خَلْقِكَ، أَوِ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الغَيْبِ عِنْدَكَ، أَنْ تَجْعَلَ القُرْآنَ رَبِيعَ قَلْبِي، وَنُورَ صَدْرِي، وَجَلاَءَ حُزْنِي، وَذَهَابَ هَمِّي)).
(Ewe Allah, mimi ni mja Wako, mwana wa mja Wako, mwana wa mjakazi Wako, utosi wangu uko mkononi Mwako (yaani una mamlaka kamili juu yangu), amri Yako juu yangu inatekelezwa daima na hukumu Yako juu yangu ni ya haki. Nakuomba kwa kila jina lililo Lako ulilojiita nalo, au ulilolishusha katika Kitabu Chako, au ulilomfundisha yeyote katika viumbe Vyako, au ulilolihifadhi katika elimu ya yasiyoonekana iliyo kwako, uifanye Qur'an kuwa uhai wa moyo wangu na nuru ya kifua changu, na kuondoa huzuni yangu na kuondoa wasiwasi wangu.)