Toba na kuomba msamaha
قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((وَاللَّهِ إِنِّي لأَسْتَغفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ فِي الْيَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةٍ)).
(Mtume wa Allah alisema: ‘Naapa kwa Allah, mimi huomba msamaha kwa Allah na hutubu kwake zaidi ya mara sabini kwa siku.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ تُوبُوا إِلَى اللَّهِ فَإِنِّي أَتُوبُ فِي الْيَوْمِ إِلَيْهِ مِائَةَ مَرَّةٍ)).
(Pia alisema: ‘Enyi watu, tubuni! Hakika mimi hutubu kwa Allah mara mia kwa siku.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ قَالَ أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ الْعَظيمَ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَيُّ القَيّوُمُ وَأَتُوبُ إِلَيهِ، غَفَرَ اللَّهُ لَهُ وَإِنْ كَانَ فَرَّ مِنَ الزَّحْفِ)).
(Pia alisema: ‘Atakayesema:(Namwomba Allah msamaha, ambaye hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliye Hai milele, Msimamizi wa vyote, na narejea kwake kwa toba.) Allah atamsamehe hata kama alikuwa mtu aliyekimbia wakati wa kusonga mbele kwa jeshi.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الرَّبُّ مِنَ الْعَبْدِ فِي جَوْفِ اللَّيْلِ الآخِرِ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَنْ تَكُونَ مِمَّنْ يَذْكُرُ اللَّهَ فِي تِلْكَ السَّاعَةِ فَكُنْ)).
(Alisema: ‘Wakati Mola alio karibu zaidi na mja Wake ni katikati ya usiku, basi ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomkumbuka Allah wakati huo, basi kuwa hivyo.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الْعَبْدُ مِنْ رَبِّهِ وَهُوَ سَاجِدٌ فَأَكثِرُوا الدُّعَاءَ)).
(Pia alisema: ‘Wakati mja alio karibu zaidi na Mola wake ni anaposujudu, basi ombeni dua nyingi humo.)
وَقَالَ صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّهُ لَيُغَانُ عَلَى قَلْبِي وَإِنِّي لأَسْتَغْفِرُ اللَّهَ فِي الْيَوْمِ مِائَةَ مَرَّةٍ)).
(Pia alisema: ‘Hakika moyo wangu hughafilika, nami huomba msamaha kwa Allah mara mia kwa siku.)(hughafilika: yaani hali ya ‘kusahau’. Mtume alikuwa daima akiongeza kumkumbuka Mola wake, kupata ukaribu na Allah na kuwa na uchaji wa Allah kiasi kwamba ikiwa makali haya yalipungua kwa namna yoyote, alikuwa akiyaona kuwa ni dhambi kisha akikimbilia kuomba msamaha kwa Allah.)