اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، اللَّهُ أَكْبَرُ، ﴿سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ وَإِنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ﴾ ((اللَّهُمَّ إِنّا نَسْأَلُكَ فِي سَفَرِنَا هَذَا البِرَّ وَالتَّقْوَى، وَمِنَ الْعَمَلِ مَا تَرْضَى، اللَّهُمَّ هَوِّنْ عَلَيْنَا سَفَرَنَا هَذَا وَاطْوِ عَنَّا بُعْدَهُ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الصَّاحِبُ فِي السَّفَرِ، وَالْخَليفَةُ فِي الْأَهْلِ، اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ وَعْثَاءِ السَّفَرِ، وَكَآبَةِ الْمَنْظَرِ، وَسُوءِ الْمُنْقَلَبِ فِي الْمَالِ وَالْأَهْلِ))، وإذا رَجَعَ قَالَهُنَّ وَزَادَ فِيهِنَّ: ((آيِبُونَ، تائِبُونَ، عَابِدُونَ، لِرَبِّنَا حَامِدُونَ)).
(Allah ni Mkubwa kuliko vyote, Allah ni Mkubwa kuliko vyote, Allah ni Mkubwa kuliko vyote. Ametakasika Yeye, Aliyetutiishia haya (chombo cha usafiri), nasi wenyewe tusingekuwa na uwezo wa hilo, na kwa Mola wetu ndiko marejeo yetu. Ewe Allah, tunakuomba katika safari yetu hii birr na taqwa, na tunakuomba vitendo vinavyokuridhisha. Ewe Allah, tufanyie safari yetu iwe nyepesi na utufupishie umbali wake. Ewe Allah, Wewe ndiye Msindikizaji katika safari na Mwakilishi juu ya familia, Ewe Allah, najikinga kwako kutokana na ugumu wa safari, kutokana na kubadilika kwa nyoyo na kuwa katika hali mbaya, na najikinga kwako kutokana na mwisho mbaya katika mali na familia.)(birr na taqwa: istilahi mbili jumuishi ambazo kila moja peke yake humaanisha matendo yote mema na utiifu, yaani kutekeleza yaliyoamrishwa na kuepuka yaliyokatazwa. Zinapokuja pamoja, birr humaanisha kufanya yale yaliyoamrishwa na taqwa humaanisha kuepuka yale yaliyokatazwa.)(Mwakilishi: ni yule anayechukua nafasi ya mwingine kwa sababu ya kutokuwepo kwake au kifo chake. Hii ndiyo maana sahihi ya neno khalifa; hivyo si sahihi kuamini kwamba Adamu ni khalifa (mwakilishi, kama inavyotafsiriwa kwa kawaida) wa Allah duniani kwa sababu Allah hayupo mbali kamwe, wala hatakufa kamwe. Dua hii inathibitisha ufahamu sahihi wa neno hili na inaonyesha kuwa Allah huchukua nafasi yetu na kuwalinda tunaowaacha tunapokufa au tunapokosekana.)(wakati wa kurudi dua hiyo hiyo husomwa kwa kuongeza yafuatayo: (Tunarudi, tunatubu, tunaabudu na tunamsifu Mola wetu.))