((الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَطْعَمَنِي هَذَا، وَرَزَقَنِيهِ، مِنْ غَيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلاَ قُوَّةٍ)).
(Sifa zote njema ni za Allah ambaye amenilisha chakula hiki na kuniruzuku bila uwezo wala nguvu kutoka kwangu.)
((الْحَمْدُ لِلَّهِ حَمْداً كَثِيراً طَيِّباً مُبَارَكاً فِيهِ، غَيْرَ [مَكْفِيٍّ وَلاَ ] مُوَدَّعٍ، وَلاَ مُسْتَغْنَىً عَنْهُ رَبَّنَا)).
(Sifa njema ziwe kwa Allah, sifa nyingi, nzuri, zenye baraka, zisizokoma, ambazo hatutaziaga wala hatuwezi kuziacha, Yeye ndiye Mola wetu.)(Kuna maoni mengine kuhusu maana ya dua hii, miongoni mwake: Sifa njema ziwe kwa Allah, sifa nyingi, nzuri, zenye baraka. Yeye ndiye Anayetosheleza, Analisha na Halishwi, Anayetamaniwa pamoja na yale yaliyo kwake, na Anayehitajiwa, Yeye ndiye Mola wetu.)