Dua za mwanzo wa swala
((اللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ، اللَّهُمَّ اغْسِلْني مِنْ خَطَايَايَ، بِالثَّلْجِ وَالْماءِ وَالْبَرَدِ)).
(Ewe Allah, niweke mbali na madhambi yangu kama ulivyoweka mbali Mashariki na Magharibi, Ewe Allah, nitakase na madhambi yangu kama vazi jeupe linavyotakaswa uchafu, Ewe Allah, nioshe madhambi yangu kwa theluji, maji na barafu.)
((سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، وَتَبارَكَ اسْمُكَ، وَتَعَالَى جَدُّكَ، وَلاَ إِلَهَ غَيْرُكَ)).
(Ametakasika Wewe, Ewe Allah, na nakusifu. Limebarikiwa jina Lako, na limetukuka daraja Lako na hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe.)
((وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ حَنِيفَاً وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ، إِنَّ صَلاَتِي، وَنُسُكِي، وَمَحْيَايَ، وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، لاَ شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا مِنَ الْمُسْلِمِينَ. اللَّهُمَّ أَنْتَ المَلِكُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَنْتَ رَبِّي وَأَنَا عَبْدُكَ، ظَلَمْتُ نَفْسِي وَاعْتَرَفْتُ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي ذُنُوبي جَمِيعَاً إِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنوبَ إِلاَّ أَنْتَ. وَاهْدِنِي لِأَحْسَنِ الأَخْلاقِ لاَ يَهْدِي لِأَحْسَنِها إِلاَّ أَنْتَ، وَاصْرِفْ عَنِّي سَيِّئَهَا، لاَ يَصْرِفُ عَنِّي سَيِّئَهَا إِلاَّ أَنْتَ، لَبَّيْكَ وَسَعْدَيْكَ، وَالخَيْرُ كُلُّهُ بِيَـــــــدَيْكَ، وَالشَّـــــرُّ لَيْسَ إِلَيْــــــكَ، أَنَا بِكَ وَإِلَيْكَ، تَبارَكْتَ وَتَعَالَيْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَيْكَ)).
(Nimeuelekeza uso wangu kwa unyofu kwa Yule aliyeumba mbingu na ardhi na mimi siko miongoni mwa wanaoshirikisha (wengine na Allah). Hakika swala yangu, kafara yangu, uhai wangu na kifo changu ni kwa Allah, Mola wa walimwengu, hana mshirika, kwa hili nimeamrishwa na mimi ni miongoni mwa Waislamu. Ewe Allah, Wewe ndiye Mfalme, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe. Wewe ni Mola wangu na mimi ni mja Wako, nimeidhulumu nafsi yangu na nimekiri dhambi yangu, basi nisamehe dhambi zangu zote kwani hakuna anayesamehe dhambi isipokuwa Wewe. Niongoze kwenye tabia njema kabisa kwani hakuna awezaye kuniongoza kwayo isipokuwa Wewe, na niokoe na tabia mbaya kabisa kwani hakuna awezaye kuniokoa nayo isipokuwa Wewe. Labbayka, nimeitikia wito Wako, nafurahia kukutumikia. Kheri yote iko mikononi Mwako na shari haitoki Kwako. Nipo kwa utashi Wako na nitarejea Kwako. Umebarikiwa na Umetukuka, naomba msamaha Wako na narejea kwako kwa toba.)(Allah haumbi shari kamili isiyokuwa na kheri yoyote wala manufaa, hekima au rehema ndani yake, wala haadhibu yeyote bila kuwa ametenda dhambi. Kitu kinaweza kuwa chema kwa upande wa uumbaji wake kinapotazamwa kwa mtazamo fulani na wakati huo huo kikawa kibaya kinapotazamwa kwa namna nyingine. Allah alimuumba shetani na kwa yeye huwajaribu waja Wake, kwa hivyo wapo wanaomchukia shetani, wanapigana naye na njia yake na wanasimama katika uadui naye na wafuasi wake, na wapo wengine wanaoshikamana na shetani na kufuata nyayo zake. Hivyo shari ipo katika viumbe Vyake kwa utashi na hekima Yake, si katika matendo Yake wala katika kitendo Chake cha kuumba.)
((اللَّهُمَّ رَبَّ جِبْرَائِيلَ، وَمِيْكَائِيلَ، وَإِسْرَافِيلَ، فَاطِرَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ، عَالِمَ الغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادِكَ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ. اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بِإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلَى صِرَاطٍ مُسْتَقيمٍ)).
(Ewe Allah, Mola wa Jibril, Mikail na Israfil (Malaika wakubwa), Muumbaji wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa yanayoonekana na yasiyoonekana. Wewe ndiye Mwamuzi kati ya waja Wako katika yale waliyokhitilafiana. Niongoze kwenye ukweli kwa idhini Yako katika yale waliyotofautiana, kwani hakika Wewe humwongoza umtakaye kwenye njia iliyonyooka.)
((اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيرَاً، اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيراً، اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيراً، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثيراً، وَسُبْحَانَ اللَّهِ بُكْرَةً وَأَصِيلاً)) ثَلاثاً ((أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ: مِنْ نَفْخِهِ، وَنَفْثِهِ، وَهَمْزِهِ)).
(Allah ni Mkubwa kabisa, Allah ni Mkubwa kabisa, Allah ni Mkubwa kabisa, sifa nyingi ni za Allah, sifa nyingi ni za Allah, sifa nyingi ni za Allah, na namtakasa Allah asubuhi na jioni.)(Najikinga kwa Allah kutokana na shetani, kutokana na kiburi chake, mashairi yake na wazimu wake.)
((اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ، أَنْتَ نُورُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ، وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ قَيِّمُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ، [وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ رَبُّ السَّمَواتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ] [وَلَكَ الْحَمْدُ لَكَ مُلْكُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَمَنْ فِيهِنَّ] [وَلَكَ الْحَمْدُ أَنْتَ مَلِكُ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ] [وَلَكَ الْحَمْدُ] [أَنْتَ الْحَقُّ، وَوَعْدُكَ الْحَقُّ، وَقَوْلُكَ الْحَقُّ، وَلِقاؤُكَ الْحَقُّ، وَالْجَنَّةُ حَقٌّ، وَالنَّارُ حَقٌّ، وَالنَّبِيُّونَ حَقٌّ، وَمحَمَّدٌ صلى الله عليه وسلم حَقٌّ، وَالسّاعَةُ حَقٌّ] [اللَّهُمَّ لَكَ أَسْلَمتُ، وَعَلَيْكَ تَوَكَّلْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَإِلَيْكَ أَنَبْتُ، وَبِكَ خاصَمْتُ، وَإِلَيْكَ حاكَمْتُ. فَاغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ، وَمَا أَخَّرْتُ، وَمَا أَسْرَرْتُ، وَمَا أَعْلَنْتُ] [وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي] [أَنْتَ المُقَدِّمُ، وَأَنْتَ المُؤَخِّرُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ] [أَنْتَ إِلَهِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ] [وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ])).
(Ewe Allah, ni Zako sifa zote, Wewe ni Nuru ya mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Ni Zako sifa zote, Wewe ni Msimamizi wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Ni Zako sifa zote. Wewe ni Mola wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Ni Zako sifa zote na ufalme wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake. Ni Zako sifa zote, Wewe ni Mfalme wa mbingu na ardhi na ni Zako sifa zote. Wewe ni Haki, ahadi Yako ni ya kweli, neno Lako ni la kweli, na Siku tutakayokutana nawe ni ya kweli, Bustani ya Peponi ni ya kweli na Moto ni wa kweli, na Mitume ni wa kweli, Muhammad ni wa kweli na Saa ya Mwisho ni ya kweli. Ewe Allah, nimejisalimisha kwako, nimekutegemea, nimekuamini, nimerejea kwako kwa toba, nimehasimiana kwa ajili Yako, na nimekuomba hukumu. Basi nisamehe yaliyopita ya madhambi yangu na yatakayokuja, niliyoyaficha na niliyoyadhihirisha. Wewe ndiye Al-Muqaddim na Al-Mu-akhkhir. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe, Wewe ndiye Mungu wangu, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe.)(Maana ya Al-Muqaddim na Al-Mu-akhkhir: Allah humtanguliza na kumpa upendeleo amtakaye miongoni mwa viumbe Vyake kama anavyomchelewesha na kumrudisha nyuma amtakaye kwa mujibu wa hekima Yake. Kwa mfano: kumpendelea mwanadamu kuliko viumbe vingine, kuwapendelea Mitume kuliko wanadamu wengine, kumpendelea Muhammad kuliko Mitume na Wajumbe wote…n.k.)
Dua wakati wa rukuu
((سُبْحانَ رَبِّيَ الْعَظِيمِ)). ثلاث مرَّاتٍ.
(Ametakasika Mola wangu, Mkuu kabisa.’(mara tatu))
((سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي)).
(Ametakasika Wewe, Ewe Allah, Mola wetu, na nakusifu. Ewe Allah, nisamehe.)
((سُبُّوُحٌ، قُدُّوسٌ، رَبُّ المَلاَئِكَةِ وَالرُّوحِ)).
(Mtakatifu na Mwenye kutakasika (Yeye), Mola wa Malaika na Roho (yaani Jibril).)
((اللَّهُمَّ لَكَ رَكَعْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، خَشَعَ لَكَ سَمْعِي، وَبَصَرِي، وَمُخِّي، وَعَــــظْمِي، وَعَصَبِي، [وَمَا استَقَلَّتْ بِهِ قَدَمِي])).
(Ewe Allah, nimerukuu kwako, na nimeamini Wewe, na nimejisalimisha kwako. Kusikia kwangu, kuona kwangu, akili yangu, mifupa yangu, mishipa yangu na kile miguu yangu inachokibeba vimenyenyekea kwako.)
((سُبْحَانَ ذِي الْجَبَرُوتِ، وَالْمَلَكُوتِ، وَالْكِبْرِيَاءِ، وَالْعَظَمَةِ)).
(Ametakasika Yeye, Mwenye nguvu kamili, ufalme, uadhama na ukuu.)
Dua wakati wa sijda
((سُبْحَانَ رَبِّيَ الأَعْلَى)) ثلاث مرَّاتٍ.
(Ametakasika Mola wangu, Aliye Juu kabisa.’(mara tatu))
((سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي)).
(Ametakasika Wewe, Ewe Allah, Mola wetu, na nakusifu. Ewe Allah, nisamehe.)
((سُبوحٌ، قُدُّوسٌ، رَبُّ الْمَلَائِكَةِ وَالرُّوحِ)).
(Mtakatifu na Mwenye kutakasika (Yeye), Mola wa Malaika na Roho (yaani Jibril).)
((اللَّهُمَّ لَكَ سَجَدْتُ وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، سَجَدَ وَجْهِيَ لِلَّذِي خَلَقَهُ، وَصَوَّرَهُ، وَشَقَّ سَمْعَهُ وَبَصَرَهُ، تَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسنُ الْخَالِقينَ)).
(Ewe Allah, nimesujudu kwako na nimekuamini, na nimejisalimisha kwako. Uso wangu umesujudu kwa Yule aliyeuumba na kuutia sura, na akatoa uwezo wake wa kusikia na kuona. Amebarikiwa Allah, Mbora wa waumbaji.)
((سُبْحَانَ ذِي الْجَبَرُوتِ، وَالْمَلَكُوتِ، وَالْكِبْرِيَاءِ، وَالْعَظَمَةِ)).
(Ametakasika Yeye, Mwenye nguvu kamili, ufalme, uadhama na ukuu.)
((اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذَنْبِي كُلَّهُ: دِقَّهُ وَجِلَّهُ، وَأَوَّلَهُ وَآخِرَهُ، وَعَلاَنِيَّتَهُ وَسِرَّهُ)).
(Ewe Allah, nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za kwanza na za mwisho, zilizo wazi na zilizofichika.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ، لاَ أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ، أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ)).
(Ewe Allah, najikinga kwa radhi Yako kutokana na ghadhabu Yako na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najikinga kwako kutokana na Wewe. Siwezi kuhesabu sifa Zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe.)
Dua baada ya tashahhud ya mwisho na kabla ya kumaliza swala
((اللَّهُــمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، وَمِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ، وَمِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ، وَمِنْ شَرِّ فِتْنَةِ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ)).
(Ewe Allah, najikinga kwako kutokana na adhabu ya kaburi, kutokana na adhabu ya Moto, kutokana na fitna na majaribu ya uhai na kifo, na kutokana na shari ya fitna ya Al-Masihi Ad-Dajjal.)(Al-Masihi Ad-Dajjal: miongoni mwa alama kubwa za Kiyama na majaribu makubwa kabisa yatakayowapata wanadamu, ambayo kila Mtume ameonya kuyahusu. Watu wengi watamfuata. Atatokea Asbahan, Iran, wakati Waislamu watakapoiteka Constantinople. Atapewa uwezo maalum na atafanya ukweli uonekane uongo na uongo uonekane ukweli. Atadai kuwa mwema, kisha atadai unabii, na mwishowe uungu. Katika sifa zake ni kwamba atakuwa kipofu wa jicho lake la kulia, jambo ambalo ni ushahidi wa wazi unaokanusha dai lake la kuwa Allah, kwani ni dalili ya upungufu. Neno Kafir litaandikwa kati ya macho yake, ambalo kila muumini, awe anajua kusoma au la, ataliona na kulitambua.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَعوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، وَأَعوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ، وَأَعوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَعوذُ بِكَ مِنَ الْمَأْثَمِ وَالْمَغْرَمِ)).
(Ewe Allah, najikinga kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na najikinga kwako kutokana na fitna na majaribu ya Al-Masihi Ad-Dajjal, na najikinga kwako kutokana na fitna na majaribu ya uhai na kifo. Ewe Allah, najikinga kwako kutokana na dhambi na deni.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْماً كَثِيراً، وَلاَ يَغْفِرُ الذُّنوبَ إِلاَّ أَنْتَ، فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ وَارْحَمْنِي، إِنَّكَ أَنْتَ الغَفورُ الرَّحيمُ)).
(Ewe Allah, hakika nimeidhulumu nafsi yangu dhuluma nyingi na hakuna anayesamehe dhambi isipokuwa Wewe, basi nisamehe msamaha utokao kwako na unirehemu. Hakika Wewe ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa rehema.)(Utokao kwako: yaani kutoka katika fadhila Yako ya ndani kabisa bila mimi kustahiki, na msamaha unaostahiki ukarimu Wako mkubwa.)
((اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ، وَمَا أَخَّرْتُ، وَمَا أَسْرَرْتُ، وَمَا أَعْلَنْتُ، وَمَا أَسْرَفْتُ، وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي. أَنْتَ الْمُقَدِّمُ، وَأَنْتَ الْمُؤَخِّرُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ)).
(Ewe Allah, nisamehe dhambi zangu zilizotangulia na zitakazofuata, nilizozificha na nilizozidhihirisha, nilizopindukia mipaka, na zile Ulizo na ujuzi nazo zaidi kuliko mimi. Wewe ndiye Al-Muqaddim na Al-Mu-akhkhir. Hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe.)(Maana ya Al-Muqaddim na Al-Mu-akhkhir: Allah humtanguliza na kumpa upendeleo amtakaye miongoni mwa viumbe Vyake kama anavyomchelewesha na kumrudisha nyuma amtakaye kwa mujibu wa hekima Yake. Kwa mfano: kumpendelea mwanadamu kuliko viumbe vingine, kuwapendelea Mitume kuliko wanadamu wengine, kumpendelea Muhammad kuliko Mitume na Wajumbe wote…n.k.)
((اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ، وَشُكْرِكَ، وَحُسْنِ عِبادَتِكَ)).
(Ewe Allah, nisaidie nikukumbuke, nikushukuru, na nikuabudu kwa uzuri kabisa.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْبُخْلِ، وَأَعوذُ بِكَ مِنَ الْجُبْنِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ أَنْ أُرَدَّ إِلَى أَرْذَلِ الْعُمُرِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الدُّنْيَا وَعَذَابِ الْقَبْرِ)).
(Ewe Allah, najikinga kwako kutokana na ubakhili na woga, najikinga kwako nisije kurudishwa katika umri mbaya kabisa “yaani uzee, udhaifu, kutokuwa na uwezo, na hali ya hofu”, na najikinga kwako kutokana na fitna na majaribu ya dunia hii na adhabu ya kaburi.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ)).
(Ewe Allah, nakuomba unipe Pepo na najikinga kwako kutokana na Moto.)
((اللَّهُمَّ بِعِلْمِكَ الغَيْبَ وَقُدْرَتِكَ عَلَى الْخَلقِ أَحْيِنِي مَا عَلِمْتَ الْحَيَاةَ خَيْراً لِي، وَتَوَفَّنِي إِذَا عَلِمْتَ الْوَفَاةَ خَيْراً لِي، اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَشْيَتَكَ فِي الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ، وَأَسْأَلُكَ كَلِمَةَ الْحَقِّ فِي الرِّضَا وَالْغَضَبِ، وَأَسْأَلُكَ الْقَصْدَ فِي الْغِنَى وَالْفَقْرِ، وَأَسْأَلُكَ نَعِيماً لاَ يَنْفَدُ، وَأَسْأَلُكَ قُرَّةَ عَيْنٍ لاَ تَنْقَطِعُ، وَأَسْأَلُكَ الرِّضَا بَعْدَ الْقَضَاءِ، وَأَسْــــأَلُكَ بَرْدَ الْعَيْشِ بَعْدَ الْمَوْتِ، وَأَسْأَلُكَ لَذَّةَ النَّظَرِ إِلَى وَجْهِكَ، وَالشَّوْقَ إِلَى لِقائِكَ فِي غَيرِ ضَرَّاءَ مُضِرَّةٍ، وَلاَ فِتْنَةٍ مُضِلَّةٍ، اللَّهُمَّ زَيِّنَا بِزِينَةِ الإِيمَانِ، وَاجْعَلْنَا هُدَاةً مُهْتَدِينَ)).
(Ewe Allah, kwa ujuzi Wako wa yasiyoonekana na uwezo Wako juu ya viumbe, nihuishe maadamu unajua uhai ni bora kwangu, na unifishe ukijua kifo ni bora kwangu. Ewe Allah, nijaalie nikuogope katika siri na hadharani, na nakuomba unijaalie nisemeje kweli wakati wa radhi na wa hasira. Nakuomba unijaalie wastani wakati wa utajiri na wa umaskini, na nakuomba neema na furaha ya daima isiyokoma. Nakuomba unijaalie kuridhika na ulichokihukumu na maisha mepesi baada ya kifo. Nakuomba ladha ya kutazama Uso Wako na shauku ya kukutana nawe, pasipo madhara yenye kudhuru wala fitna yenye kupoteza. Ewe Allah, tupambe kwa pambo la imani na utujaalie kuwa miongoni mwa wanaoongoza na walioongoka.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ يَا أَللَّهُ بِأَنَّكَ الْوَاحِدُ الْأَحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يولَدْ، وَلَمْ يَكنْ لَهُ كُفُواً أَحَدٌ، أَنْ تَغْفِرَ لِي ذُنُوبِي إِنَّكَ أَنْتَ الْغَفُورُ الرَّحِّيمُ)).
(Ewe Allah, nakuomba Ewe Allah, kwa kuwa Wewe ni Mmoja, Wa Pekee, As-Samad, Ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa na hakuna anayefanana naye, unisamehe dhambi zangu, kwani hakika Wewe ndiye Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa rehema.)(As-Samad: Bwana Asiyehitaji chochote, Mwenye sifa kamilifu ambaye viumbe vyote humwelekea katika mahitaji yao yote.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَمْدَ لَا إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ وَحْدَكَ لاَ شَرِيكَ لَكَ، الْمَنَّانُ، يَا بَدِيعَ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ يَا ذَا الْجَلاَلِ وَالْإِكْرَامِ، يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ)).
(Ewe Allah, nakuomba kwa kuwa sifa zote ni Zako, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe, peke yako, huna mshirika. Wewe ndiye Mpaji. Ewe Muumbaji wa mbingu na ardhi, Ewe Mwenye utukufu na heshima, Ewe Uliye Hai milele, Ewe Msimamizi wa vyote, hakika nakuomba Pepo na najikinga kwako kutokana na Moto.)
((اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِأَنَّي أَشْهَدُ أَنَّكَ أَنْتَ اللَّهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ الْأَحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُواً أَحَدٌ)) .
(Ewe Allah, nakuomba, kwa kuwa nashuhudia kwamba Wewe ni Allah, hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Wewe, Mmoja, As-Samad, Ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa na hakuna anayefanana naye.)(As-Samad: Bwana Asiyehitaji chochote, Mwenye sifa kamilifu ambaye viumbe vyote humwelekea katika mahitaji yao yote.)